Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mimi Mars amefunguka na kusema kuwa, hana mahusiano ya kimapenzi na msanii mwenzake, Marioo bali ni marafiki tu.
Mimi Mars amesema hayo wikiendi iliyopita katika uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya wa La La aliyomshirikisha Marioo.
Mimi Mars anasema; “Sisi tupo kwenye mahusiano ya urafiki, but imekua imefikia hatua watu wanasema ni mahusiano ya kimapenzi…”
Kama utakumbuka, Wimbo wa La La ni wa pili kwa Mimi Mars kumshirikisha Marioo, wa kwanza ni Una ambao alimshikisha pia Young Lunya alikuwepo.