Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Tunda Man amemshukuru mwanamuziki mwenzake Harmonize baada ya kumsaidia kufanya wimbo wa pamoja unaokwenda kwa jina la Badman.
Baada ya ngoma ya Badman ya Tunda Man aliyomshirikisha Harmonize kufanya vizuri ameandika kwenye Instagram yake kuwa:
”Asante mdogo wangu Harmonize kwa hizi pongezi ila ww ndio unahitaji pongezi nyingi zaid kwenye hii heshima kubwa ninayopewa kwenye nchi yangu na nchi zingine.
Wewe mdogo wangu Harmonize umeweza kuni prove wrong kuwa trending NO: 01 anakaa mtu yeyote mi nilijua namba moja ni kwa watu wachache tu. Thanx kwa kujitoa kusurpot ngoma niliyokushirikisha kama yako nimefika NO: 1 mpka Qatar nchi yenye kombe la dunia bila kuandika barua.
Wengi wanakupiga vita ila hawajua wanaempiga vita analindwa na moyo wake mwema ALLAH hawez kukuacha peke yako niamini.
Tunda ameongeza “Watu unaowasaidia pale kwako bila camera bila promo pamoja na mm nikiwemo ni jambo kubwa na ALLAH Atakupa mara mbili zaidi. Thanx kwa kunipambania na sikulipi chochote ila kuwa na moyo huo huo maana moyo wako ndio kinga yako!! Mi naamini MTI WENYE MATUNDA…..