Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amepokea ushindi wake wa tuzo ya mjasiriamali bora wa mwaka ya mwaka 2021.
Shilole kwa picha akipokea ushindi wa tuzo hiyo ya kipengele Cha ‘Best Entrepreneur on the Digital (2021) kwenye Tanzania Digital Awards kwa mara ya pili mfululizo alieleza furaha yake na kuitaja kuwa tuzo kubwa kwake..
Kwenye ujumbe wake kupitia ukurasa wake wa Instagram pia Shilole amewashukuru wote wanaomshika mkono wakiwemo mashabiki wanaofuatilia kazi na jitihada zake zaidi kupitia biashara yake ya mgahawa wake maarufu, ‘Shishi Food’.
Aidha Shilole ameongeza kuwa ushindi huo kwa mara ya pili mfululizo ni matokeo chanya ya ya matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii na kushauri jamii kuitumia pia mitandao kwa manufaa kwakuwa ni njia kati ya zile Bora katika kujitangaza kibiashara.