Penzi ambalo awali lilivunjika kati ya staa wa Bongo Movie, Kajala na Harmonize ni kama limerejea upya baada ya Kajala kumuondolea ‘block’ Harmonize ambaye walipoachana alimblock kwenye akaunti yake ya Instagram.
Katika tukio jipya, leo Kajala ametupia picha yake kali kwenye akaunti yake ya Instagram na kusindikiza na maneno: “I mind my own business & talk to God a lot…” akimaanisha nafanya mambo yangu na kuzungumza sana na Mungu”.
Muda mfupi baadaye, Harmonize aliibuka na kuweka comment chini ya post hiyo ya Kajala kwa kuandika: “Tanzania Number Actress, Harmonize Wife & Manager” akimaanisha ‘Msanii wa filamu wa kike namba moja Tanzania, mke wa Harmonize na Meneja.’
Comment hiyo imezua mjadala mkubwa ikionesha kwamba wawili hao wamezama tena penzini baada ya awali jini mkata kamba kulipitia penzi lao na hii inakuja baada ya Harmonize kutumia nguvu kubwa kujaribu kumshawishi Kajala warudiane.