Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuchu ametoa taarifa kuwa amepata ajali siku moja kabla ya kufanya show yake nchini Ningeria.

Imekuwa ni siku mbaya kwa mwanamuziki kutoka lebo ya WCB, Zuchu hii ni baada ya kuripoti kuwa amepata ajali ikiwa ni siku moja kabla ya kwenye show nchini Nigeria.

Kupitia akaunti yake ya mtandao wa twitter zuchu ameandika jumbe mbalimbali akiambatanisha na majeraha aliyoyapata sehemu ya goti baada ya kupata ajali hiyo.

Zuchu ameanza kwa kuposti kuwa “I’m sad today and confused  it’s not my habit to share my struggles but well here i go“.

Ameandika kuwa Nimepata Ajali ndogo iliyo umiza goti langu jana siku moja kabla ya safari yangu kwenda kuperform Kwenye show Ya Muhimu kwangu nchini Nigeria .Canceling a show is one of the hardest decisions siwezi as an artist leo ndo nimejua

Pia ameandika My manager keeps telling me Afya ni muhimu ila najua ntajiskia vibaya zaidi kutaka kucancell kwenye show kama hii naona bora nikapambanie stagini so pray for me .Am hurt and confused.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *