Wimbo mpya wa Maua Sama anaotarajia kuachia siku za usoni utakaokuwa na jumla ya dakika 23 utaweka rekodi ya wimbo mrefu zaidi kuwahi kutokea kwenye historia ya muziki wa Bongo fleva.

Maua Sama amefunguka mapya kuhusu matayarisho ya wimbo huo ikiwamo kumtaja Executive producer wa mradi huo wa wimbo wenye dakika 23, ambaye ni mwanamuziki na mbunge wa Muhezi Hamis Mwinjuma maarufu MwanFa.

“Dear GODFATHER, Hon Hamis Mwinjuma ,(MP) Mwana Fa kwanza nikushukuru kwa kila kitu. Uliamini katika Kipaji changu na kufanya mziki kuwa ajira yangu. UMENIPAMBANANIA Sana.

Katika kipindi chote hukuchoka na uliamini nitafanya uwe proud kwa maamuzi yako ya kunieleta mjini.

Kwenye track ya Dk 23 za CINEMA ukaamua kutumia Pesa zako, Ubunifu, muda wako mbali na majukumu magumu ya kuwatumikia Wananchi wa Muheza, na mpaka kuamua usitoe Ngoma mpaka nikamilishe project Yangu. Asante sana” ameandika Maua

Maua pia amemtaja mtayarishaji mahiri wa muziki nchini Hermy B kama muongozaji wa mradi huo ‘Music Director” kwa kuweka kidogezo cha kionjo cha mtayarishaji huyo.

“Kwenye Track hii ya Hermy B 23 Minutes, Zilikuwa Dk 49 lakini zikapunguzwa mpaka kufika 23! Kuna wakati nilijua hatuwezi kumaliza hii Kazi Maana kila siku yalikuwa yanaletwa makosa mapya.

Yaliyonilazimu lazima niende tena studio S/O to my Brother from another Mother Hermy B. wakati unaendelea kuEnjoy na video ya Baba Jeni, Ngoma yetu ya Dk 23 iko tayari” ameongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *