Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Linah amefunguka na kusema kuwa akiwa na mpenzi ni lazima amuombe pesa kwa sababu ni jukumu lake kumhudumia na haoni aibu hata tone.
Linah amesema kuwa, mwanaume anawajibu wa kumhudumia mpenzi wake kwa kila kitu bila hata kuombwa.
Kuna baadhi ya wanaume wanasema kuwa wao hawawezi kuwahonga wapenzi wao pesa, jamani kama ndiyo hivyo pisi kali zote watazisikia tu redioni, binafsi nikiwa na mpenzi wangu namuomba pesa ya kila kitu kwa sababu ni jukumu lake kunihudumia na sioni hata aibu kwa hilo,” anasema
Linah ni mama wa mtoto mmoja ambaye bado ngoma yake na Kayumba ya Umeniweza inagusa mioyo ya mashabiki wake.