Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuwa kamwe hawezi kuchora tattoo ya jina la mwanaume kwenye mwili wake kwa sababu hakuna mwanaume wa kumuamini zaidi ya mzazi wake ambapo yeye amemchora baba yake mzazi, marehemu Balozi Sepetu.

Wema amesema kuwa, hakuna kitu ambacho mwanaume anaweza kumfanyia chenye maajabu makubwa kwake kiasi cha kumchora tattoo.

Hivyo kamwe hawezi kuchora jina la mwanaume yeyote kwenye mwili wake zaidi ya wazazi wake au watoto wake akibarikiwa na si vinginevyo.

Amesema kuwa “Yaani mwanaume ambaye nimempa nafasi ya kumchora mwilini wangu ni baba yangu peke yake na si mtu mwingine yeyote maana sijaona maajabu aliyofanya mwanaume kwangu mpaka niende kabisa kumchora na hata akiyafanya bado hana nafasi ya kumchora kwenye mwili wangu kabisa maana hata kwa Mungu nitaulizwa juu ya hilo,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *