Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu imepanga Mei 31, 2022 itatoa hukumu ya kesi ya kusambaza picha za utupu inayomkabili msanii wa maigizo, Mwemba Burton maarufu kama Mwijaku.
Hiyo ni baada ya Mwijaku na wenzake wawili kumaliza kutoa ushahidi wao na kisha kufunga ushahidi wa upande wa utetezi leo Jumatano Mei 11, 2022.
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Rhoda Ngimilanga amepanga tarehe hiyo baada ya mashahidi hao wa upande wa utetezi kumaliza kutoa ushahidi wao.
“Nitatoa hukumu Mei 31, 2022 na mshtakiwa utaendelea kuwa nje kwa dhamana” amesema Hakimu Ngimilanga.
Mwinjaku alikutwa na kesi ya kujibu wiki iliyopita baada ya mahakama kupitia ushahidi wa mashahidi watano na vielelezo vinne vilivyotolewa na upande wa mashtaka.