Mwanamuziki wa Singeli, Balaa MC amefunguka na kusema kuwa anatarajia kuachia albam yake mpya na mipango imekamilika tayari hivyo hivi punde itaingia sokoni.
Nipende kuchukua nafasi hii kukushukuru wewe shabiki yangu, wewe ambae unaupenda mziki wa Singeli na wale wote ambao kwa namna moja au nyingine wamehusika kwenye hii safari yangu ya mziki tangia nianze 2020 mpaka kufikia kuandaa Album ya 26 Kipaji, niseme ASANTE.
Matumaini yangu 26 Kipaji Singeli Albam ndio album ya Singeli ambayo itakwenda kuongeza thamani ya mziki wa Singeli na Kutuvusha stage moja kwenda nyengine na kufanya mziki wetu ukakua Zaidi ndani na nje ya Tanzania.
Mwisho nikiombe sana support yako Ili kukamilisha haya yote mpaka pale Album itakapotoka. Nawapenda sana.