Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ametangaza kuwa video inayofuata ni ya wimbo wake wa Sona aliomshirikisha mwanamuziki wa Nigeria Adekunle ambapo wimbo huo unapatikana kwenye EP yake ya FOA.

Diamond Platnumz ataachia video ya wimbo huo aliomshirikisha Adekunle kutokea Nigeria kesho April 6, ikiwa ni video ya nne kutoka kwenye EP hiyo aliyotoka Machi 11 2022.

Video hiyo itafuata baada ya video ya ‘Fine’, ‘Mtasubiri’ aliyomshirikisha Zuchu na ‘Wonder’ ikiwa zimesalia video za nyimbo 6 kukamilisha nyimbo 10 za EP hiyo ya Diamond.

Mwanamuziki huyo anaendelea kufanya vizuri na EP yake hivyo amewataka mashabiki wake kuendelea kusapoti kazi zake ili aendelee kufanya vizuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *