Mtangazaji wa kituo cha radio, Mwemba Burton maarufu Mwijaku amekutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Mwijaku ambaye ni maarufu katika mitandao ya kijamii amekutwa na hatia na ataanza kujitetea mahakamani kutokana na kosa lake.
Ni baada ya Serikali kufunga ushahidi wao wa mashahidi watano na vielelezo vinne walivyoviwasilisha wakati wa ushahidi.
Mwijaku anakabiliwa na shtaka moja la kusambaza picha za utupu kinyume cha sharia hivyo mahakama imemkuta na hatia ya kujibu mtangazaji huyo.