Mwanamitindo maarufu wa kimataifa wa Tanzania, Miriam Odemba amefunguka na kusema kuwa anataka apelekewe mimba zote za wanawake wanaodaiwa kupewa na Ibrah.
Odemba ambaye kuna tetesi kwamba anatoka kimapenzi na msanii wa Konde Gang, Ibraah ametoa kali ya mwaka baada ya kutaka apelekewa mimba zote za wanawake wanadai kupewa ujauzito na jamaa huyo.
Amesema; “Kuanzia leo tarehe 4 mwezi wa tano mwaka elfu mbili na ishirini na mbili natangaza kwamba napokea mimba zote ambazo Chinga (Ibraah) amewapa wasichana mbalimbali pamoja na watoto aliozaa na wasichana wengine nje, wala msiogope jitokezeni kwa wingi kwa kuwa mimi ni mwanamke.
“Mimi ni mpenzi na mimi ni mama naweza kulea watoto, naweza kulea familia, uwezo wa kuwapeleka shule ninao, uwezo wa kuwalisha ninao, uwezo wa kuwakatia bima ya afya ninao, uwezo wa kuwapeleka outing ninao na mahitaji mengine yote muhimu naweza kuwapa hivyo acheni kumuumiza kichwa mume wangu Chinga keep focusing my meme i’m done. i missed your fourty seven (47).”
Kauli ya Odemba inakuja kufuatia kuibuka kwa mwanamke anayedai kuzaa na Ibraah ambaye anadai jamaa huyo hatoi matunzo ya mtoto.