Kundi la muziki nchini, Navy Kenzo wamesema kuwa albamu yao mpya imekamilika kwa asilimia 95, ambapo pia wametaja jina la albamu hiyo mpya kuwa Dread and Love.

Hii ni albamu yao ya nne ya Studio baada ya ‘Hold Me Back 2015, AIM (Above in A Minute 2017 na Story of African Mob 2020’ ambazo zimefanya vizuri sokoni.

Mmoja wa mwanamuziki anayounda kundi hilo Nahreal amesema kuwa albam hiyo imekamilika kwa asilimia mia moja hivyo mashabiki wao wakae mkao wa kula kuipokea albam yake hiyo.

Albam hiyo itatoka hivi karibuni baada ya kukamilika kwani kila kitu kimekwenda kama kilivyopangwa hivyo mashabiki wanatakiwa kuipokea na kuisapoti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *