Mzazi mwenza wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny aitwae Fayvanny amefunguka na kusema kuwa sasa amerudisha mpenzi wake huyo kwenye himaya yake baada ya kutengana.
Fahyma alitengana na Rayvanny au Chui kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu baada ya kutuhumiana kwa usaliti ambapo jamaa huyo aliangukia kwenye penzi la Paula Kajala; binti wa mwigizaji Kajala Masanja.
Fahyma sasa anatamba kwamba hatimaye amefanikiwa kulirudisha penzi lake na Rayvanny ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydanny.
Kinachoendelea kwa sasa kwa Fahyma ni kushangilia tu na kufanya sherehe huku baadhi ya watu wakisema ameanza kunenepa baada ya kutoka kwenye msongo wa mawazo na kujihakikishia ndiye mama mjengo.
Kupitia Insta Story yake huku akisikiliza Wimbo wa Mama la Mama wa Rayvanny aliomshirikisha Mr Bule, Fahyma anasema; “Aaa…weee mama la mama sina mwingine zaidi yako…”
Kufuatia ishu hiyo, timu yake wameendelea kumpongeza mno Fahyma kwa hatua aliyofikia huku wakimsisitiza kufunga ndoa na Rayvanny moja kwa moja ili ieleweke kabisa kwamba ni wanandoa na kama kuna mwanamke atakuwa anamtaka jamaa huyo basi ajue ni mume wa mtu wa ndoa kabisa.