Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja ameendelea kumchunia mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize licha ya kuombwa msamaha.
Kajala ameposti picha yake tamu na mpya kisha akaandika; “Ni rahisi mno kutafuta mtu mpya, lakini ni ngumu kumpata mkweli au mwenye mapenzi ya dhati…”
Ujumbe huo umekuja muda mfupi baada ya mmoja wa mashabiki wa Harmonize kujichora tattoo yenye ujumbe wa kumuomba Kajala amrudie Harmonize.
Harmonize amekuwa akimuomba Kajala amsamehe na kumrudia, lakini mwanamama huyo ameweka ngumu.
Kuachana kwa Kajala na Harmonize kulitokana na ile skendo maarufu ya ‘washa taa’ ambapo jamaa huyo alidaiwa kumtaka kimapenzi binti wa Kajala, Paula Kajala ili ale kuku na mayai yake.