Mwanamuziki wa Bongo Fleva, County Boy amefungua lebo yake ya Muziki ambayo ameipa jina la I am Music Co ambayo itakuwa inasimamia wasanii wa Bongo Fleva ambao wanachipukia.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Counrty ameitambulisha lebo hiyo kwa ambayo itakuwa tayari kusimamia wasanii mbali mbali nchini.
Kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika
“Kutokana na jitihada anazozionesha
Rais wetu mpendwa,Mama etu kipenzi MH SAMIA SULUHU HASSAN kuhakikisha Nchi yetu inasonga mbele mimi kama kijana sijataka kubaki nyuma Nimefungua kampuni iitwayo @iam_music_co Ambayo itahusika katika kusaidia vijana Mtaani ambao wengi wanataman kutimiza ndoto zao lakin wanashindwa kutimiza kutokana Na changamoto wanazokutana nazo hvyo basi Nakuja mbele yenu Watanzania na serikali kwa ujumla kuipokea KAMPUNI hii.
Pia amemaliza kwa kuandika Hatuna pesa nyingi lakin Tunaamin katika kidogo tulichonacho Kitatuvusha kutoka sehem Moja kwenda Nyingne.