Baada ya mwanamuziki wa Rap, Young D kutoa diss track aliyowachana wasanii wenzake, Young Killer na Stamina ambapo mistari ya ngoma hiyo inasema Kuwa Alale Pema Stamina Kwa Maana Ya Kuwa Amekufa Kimuziki.
Stamina amesema kuwa yeye hawezi kubishana na mtu ambaye anamzidi kila kitu kwenye muziki hivyo hana muda mchafu kuifuatiliwa ngoma hiyo.
Stamina amesema kuwa “Kwangu Siitafsiri Kitu Kwasababu Anaposema Kwamba Ulale Salama Kwamba Mimi Nimeshakufa Mi Sishangai Kwa Maana Yeye Ndio Maiti Sasa Nashangaa Maiti Inaongea Ndio Maana Sikushangaa Nikaona Bora Niendelee Tu Na Shughuli Zangu”.
“Ujue Kwasasa Dunia Inaenda Na Numbers Tusiongee Sana Tuache Numbers Ziongee Kwahiyo Nikiangalia Numbers Naona Sina Cha Kubishania, Ametoa Album Juzi Na Mimi Nimetoa Album Juzi Album Yangu Ina Streams Milioni .
Pia amesema kuwa Wimbo Wangu Wa Mwisho Wa Baba Youtube Una Views Karibia Milioni 4 Huko Sasa Nianze Kuongea Nini Tena Nibishane Na Mtu Kwa Mdomo?? Tubishane Kwa Numbers Mzee”
Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa Sasa Kwanini Niendelee Kupoteza Muda Wangu Hata Liwekwe Biti Hapo Waseme Chaneni Still Hawezi Kutoboa Kweli Nianze Kuhangaika Na Mtu Kama Huyo? Nina Vitu Vingi Vya Kufanya”.