Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Afande Sele amefunguka na kusema kuwa kabla ya kifo cha Maunda Zorro alipeleka mahari kwa Mzee Zahir Zorro kwa ajili ya mdogo wake kutaka kumuoa lakini bahati mbaya akafariki.

Afande Sele amesema hayo wakati wa msiba wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Maunda Zorro uliofanyika Kigamboni.

Afande Sele amesema kuwa “Maunda Zorro mimi ni familia yangu, mahari yake nimepeleka kwa Mzee Zorro na Banana Zoro, tukawakabidhi pesa tukisubiri harusi lakini kwa bahati mbaya M/mungu kafanya kazi yake”.

Pia ameongeza kusema aliongea na Maunda wiki moja kabla ya kifo chake ambapo walipanga kusherekea pamoja sikukuu ya Pasaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *