Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka na kusema kuwa amepitia kipindi kigumu sana baada ya akaunti yake ya Instagram kudukuliwa wiki chache zilizopita.
Nandy amefunguka kwa Mara ya kwanza hali alikuwa akiiptia kipindi anapambana kuirudisha akaunti hiyo huku akisema kuwa Mpenzi wake Billnass alikuwa yupo tayari kumpatia akaunti yake ya Instagram ili ampe amani.
“Haikuwa rahisi kuweka smile Kwenye nyuso za watu wangu wa karibu while nilikuwa napitia wakati mgumu alisema Nandy baada ya kurudisha akaunti yake hiyo.
Hii account ni NUSU ya mafanikio yangu ya mziki! Shukrani za dhati kwa TCRA na business partners wangu Empawa Africa bila kumsahau kipenzi chake Billnass masikini ulikuwa uko tayar kabisa kuniachia account yako ili tu niweke amani na furaha Kwenye uso wangu Nakupenda sana na ASANTE kwa kuwa na mimi kwa kipindi hichi!
Kwasasa amefanikiwa kuirudisha akaunti yake hiyo na kuendelea kuitumia kama zamani baada ya kurejea tena hewani baada ya kudukuliwa.