Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole ametimiza mwaka mmoja wa ndoa na mpenzi wake Rommy 3D ambapo ndoa hiyo ilifanyika tarehe kama ya leo mwaka jana.

Wawili hao kwa pamoja wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kutumiana jumbe za upendo kama sehemu ya kusherehekea mwaka mmoja wa ndoa yao.

Shilole ameenda mbali zaidi na kudokeza kuhusu historia fupi ya penzi lao, wakati waliokutana, kuachana na kurudiana tena mapaka hatma ya kufikia uamuzi wa kuwa wanandoa.

Mungu ndiye muandishi wa hadithi za maisha yetu, yeye mwenyewe anajua kwa nini tulitengana na kwa nini nilipitia yote niliyopitia kabla ya kukutana tena na mume wangu.

Ninachojua mimi, kukutana tena na Rommy na kufunga naye ndoa ni zawadi kubwa zaidi niliyokirimiwa na Allah.

Ndoa hii ndio nilichotaka, Mume huyu ndiye niliyestahili, hata wakati ule ‘mnabet’ kuwa ndoa itadumu mwezi mmoja na mimi nilimuachia Mungu aamue hatma yetu kwa rekhma zake.

Tuko hapa kwa uwezo wa Mungu na yeye Inshaalah ataendelea kulinda ndoa yetu.

Tunamshukuru Mungu leo tunapotimiza mwaka mmoja wa ndoa yetu. Namshukuru Mume wangu kwa kuendelea kuwa mume bora kwangu na kiungo muhimu cha furaha kwetu. nakupenda sana Mume wangu,” ameandika Shilole.

Kwa upande wa mume wa Shilole Rommy 3D yeye ameweka wazi mambo kadhaa kuhusu magumu waliyoyapitia na namna walivyojikita katika kutimiza lengo la wao kuingia kwenye ndoa bila kusikiliza maneno ya watu ambao kundi kubwa lilikuwa likitabiri kuwa pengine wawili hao hawatafika popote.

“Siku ya leo tunasherehekea mwaka mmoja wa ndoa yetu najua kinaweza kua ni kipindi kifupi ukilinganisha na watu wengine ambao wamekaa miaka mingi zaidi ndani ya ndoa zao lakini kwa upande wangu siku 360 ni nyingi sana kuweza kusherehekea katika ndoa yangu kwa sababu sio rahisi kama inavyoonekana hasa ukizingatia mke wangu ni mtu maarufu ambae anapendwa karibuni na kila mtu (Alhamdulillah).

Kukatishwa tamaa, kudharaulika, kupingwa kutabiriwa mabaya ndio imekua style ya maisha yetu lakini Mungu ni mkubwa kuliko chochote still tuko pamoja na Inshallah tuna miaka mingi mingine inakuja kwa kua Mungu anatupigania, mke wangu Shilole nakupenda sana,” ameandika Rommy kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *