Msanii wa filamu aliyezaa mtoto na Barakah The Prince, Careen Simba amesema kuwa chanzo cha kuachana na msanii huyo ni kuanzisha mahusiano na Naj wakati akiwa na ujauzito wake.
Careen Simba ambaye pia ni video vixen anasema “Mimi na Barakah tulijuana muda mrefu sana, mimi mpaka nabeba mimba tukaachana na Barakah na kuzinguana kwa sababu ya Naj, sikuwa mchepuko nilikua mwanamke wake”.
Careen Simba ameongeza kusema wakati yupo kwenye mahusiano na Barakah hawakutaka kuweka wazi kwa sababu hapendi mambo ya kujulikana sana.
Wawili hao kwasasa hawapo pamoja kutokana na kila mmoja akiwa na mahusiano yake mengine hivyo kila mmoja ana angalia maisha yake.