Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny ameondoa utambulisho wake wa kuwa chini ya lebo ya WCB chini ya Diamond Platnumz kwenye Bio ya ukurasa wake wa Instagram.
Hatua hiyo ya Rayvanny inaachia maswali yanayoweza kuwapa nafasi baadhi ya mashabiki wa muziki na wafuatiliaji wake kuamini kuwa Msanii huyo kwa sasa hafanyi kazi chini ya lebo hiyo iliyosaini naye mkataba wa kibiashara mwaka 2016.
Mwanamuziki huyo anamiliki lebo ya Next Level Music inaonekana kuwa yupo mbioni kuachana na lebo ya WCB ambayo ndio iliyomtoa kimuziki mwaka 2016 kupitia wimbo wake wa kwanza ‘Kwetu’.
Rayvanny amekuwa mwanamuziki mwenye mafanikio ndani ya lebo hiyo toka ajiunge na lebo hiyo ya WCB chini ya Diamond Platnumz ambapo sasa anaonekana yupo mbioni kuachana nayo.