Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Baby Madaha amefunguka ukaribu aliokuwa nao na msanii ambaye kwa sasa ni marehemu Maunda Zoro.
Madaha amedai Maunda alikuwa na tatizo la kiimani ambapo siku mbili kabla ya kifo chake alimuambia kuwa hajisikii vizuri, kwani anaota ndoto za ajabu ajabu na akaomba kama itawezekana basi apate msaada wa maombi kutoka kwa mchungaji.
Pia Baby Mada amesema kuwa yeye pamoja na Meneja wake walifanya jitihada za kumuunganisha na Mchungaji na akafanikiwa kuongea naye kwa njia ya simu na kumuelezea changamoto alizopata ambapo mchugaji alipanga muda wa kuonana ili ampatie huduma ya maombi lakini ilipofika siku hiyo Maunda Zorro hakuweza kupokea simu.
Baby Madaha amemuelezea marehemu Maunda Zorro kama mtu aliyekuwa na roho nzuri mchangamfu na mwenye upendo kiasi kwamba aliweza kuwa rafikiyake mkubwa na hadi sasa haamini kama kweli hayupo naye tena.