Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy ametolea ufafanuzi suala la yeye na Billnass kuacha Muziki baada ya ndoa yao kufanyika.

Dhana hiyo iliyopo kwa baadhi ya mashabiki wake kuhusu ndoa anayotarajia kufunga siku za usoni na msanii mwenzie rapa Billnas.

Labda niseme tu kwamba mimi ndio nitakuwa mfano wa yule mwanamuziki ambaye natokea Afrika mashariki au Afrika ambaye ameingia kwenye ndoa, tena ndoa takatifu lakini muziki wake upo pale pale namba moja so tuendelee kuombeana, mambo mazuri yanakuja, kuna maisha baada ya muziki.” Alisema Nandy

Nandy aliongeza kuwa, yeye ni binti na kuna hatua lazima azipige pamoja na kuwa msanii na ni vyema kuvitimiza hata kama ni mwanamuziki.

Nandy na Billnas kwa sasa wako katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa taratibu za kuelekea kufunga ndoa, ambapo mapema Februari 20, 2022 ilikuwa ni siku ambayo rapa Billnas alifanikiwa kutoa mahari kwa wazazi wa Nandy tayari kwa kung’oa jiko.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *