Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja ameonekana hana nia ya kurudiana na mpenzi wake wa zamani Harmnize licha ya mwanamuziki huyo kuomba msamaha.
Kajala amekuwa akitoa jumbe mbalimbali ambazo zimekuwa zikitafsiriwa kama majibu yasiyo ya moja kwa moja kuhusiana na ombi hilo.
Kwa mfano; kupitia Insta Story yake, Kajala ameandika; “No one knows what you feel inside’.
Mashabiki wa Harmonize wamesema kuwa wamevuta pumzi kidogo kwa ujumbe huo kwani huwenda mwanamama huyo ameanza kuelewa ombi la Harmonize.
Harmonize amekuwa akitrendi baada ya kuanza kupigana juu chini ili aweze kurudiana na Kajala waliyeachana mwaka jana.
Harmonize amesema kuwa amejaribu kuukimbia ukweli wa kimapenzi kwa kwenda zake kuanzisha penzi jipya na mwanamke kutoka Australia, Briana ila bado moyo wake umekataa kusonga mbele, badala yake umebaki katika gereza la Kajala.