Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ruby amezua taharuki kote mitandaoni muda mfupi baada ya kuweka chapisho kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akiashiria kuwa anapitia wakati mgumu kwenye maisha yake kiasi cha kutamani kufa.

Kupitia akaunti yake ya Instagram ameadika “Najisikia tu nife nikapumzike na ya dunia.” Maneno ambayo yamezua taharuki.

Aidha kufuatia ujumbe huo uliowashtua watu mbali mbali, mwanamitindo maarufu nchini Flaviana Matata ameutumia ukurasa wake wa mtandao wa twitter kutoa rai kwa yeyote aliyekaribu na Ruby kuhakikisha anampatia msaada ili kuepuka athari zaidi.

“Yeyote aliyekaribu na Ruby anapaswa kuhakikisha anapata msaada kabla ya kuchelewa. Tafadhali” ameandika Matata.

Mpaka sasa haijajulikana ni nini kinachomsibu Ruby mpaka kupelekea kuandika hivyo katika ukurasa wake wa Instagram.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *