Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Juma Jux ameweka msisitizo kuwa hatomuacha mpenzi wake licha ya kuvumishwa kwa taarifa kuwa kwa sasa penzi lake limevunjika.

Jux aliweka msisitizo huo kupitia Insta Story yake baada ya uvumi huo uliosambazwa wa penzi kuvunjika ukiambatanishwa kwa taarifa ya Karen kwenye mtandao wa Instagram.

Bila kumtambulisha wazi mpenzi wake kama kawaida yake kwenye penzi lake la sasa Jux alieleza hilo ikiaminika ni ujumbe unaomhusu mrembo aliyemfanyia ‘surprise’ ya mahaba siku ya wapendanao mwaka huu.

Mwanamuziki huyo ameingia kwenye mahusiano hayo baada ya kuachana na mpenzi wake Vanessa Mdee ambaye kwasasa yupo kwenye mahusiano na Rotimi raia wa Nigeria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *