Mwanamiziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka na kusema kuwa hawezi kushika na kukagua simu ya mpenzi wake kwani kila mmoja ana mipaka yake.

Nandy amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni yake ya Funguka ambapo alikutana na vijana mbalimbali na kueleza matatizo yao na pia kuyatafutia namna ya kuyatatua.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa katika mahusiano akiwekeana mipaka inakuwa vizuri kwani kushika simu ya mpenzi wako inaweza kuleta migogoro katika mahusiano husika kwa upande wake afanyi hivyo.

‘Mimi siwezi kushika simu ya mpenzi wangu na kuanza kukagau kwani vitu hivyo vinaaribu sana mahusiano ya kimapenzi’ Alisema Nandy

Pia Nandy ameeleza baadhi ya changamoto alizokutana nazo baada ya shabiki kuleta sintofahamu wakati akiongea naye Insta live.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *