Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize ameendelea kumuomba msamaha mpenzi wake wa zamani ambaye ni muigizaji Kajala Masanja baada ya kukiri makossa yake.

Harmonize amekuwa hang’ati maneno; anachotaka ni kumuona Kajala akirejea kwake na kuwa mkewe hivyo hasikii la kuambiwa.

Harmonize amekwenda mbali kiasi cha kumuwe Kajala kwenye bango pale Kinondoni-Manyanya yapata wiki moja sasa na litakaa hapo kwa muda wa miezi sita na kugharimu shilingi milioni 12.

Lakini hayo yote ni cha mtoto, Harmonize amekwenda mbali zaidi na kumuomba msamaha hadi binti wa Kajala, Paula Kajala kuhusiana na ile skendo ya ‘washa taa’ ambapo iliwafikisha hadi Polisi.

Harmonize anaahidi kuwa baba bora kwa Paula na atamchukulia mpenzi wake ambaye ni msanii Rayvanny kama mwanawe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *