Muigizaji wa Bongo Fleva, Wema Sepetu amesema watu waache kufuatilia maisha yake kwani kila mtu ana maisha yake hivyo siyo vizuri kufuatiliana.
Wema amesema kuwa anashangaa watu wanavyomjadili utafikiri wameona kitu gani cha ajabu, wakati yule ni rafiki yake tu kama walivyo rafiki zake wengine.
“Mimi sijaona tatizo kwenye ile video, tulikuwa sehemu tuna-enjoy na Davito ni mshikaji wangu, sasa sijui cha ajabu nini hapo, sitaki kufuatiliwa maisha yangu, naomba waniache kwa sababu siku zote siwezi kuishi vile ambavyo wao wanataka,” anasema Madam Wema.
Muigizaji huyo anatambulika kama muigizaji mwenye mvuto katika tasnia ya Bongo Movie kutokana na uhodari wake wa kuigiza.