Mwananchi wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesema uwa hapendezwi kushindanishwa na wasanii nchini kutokana na kuwazidi katika maeneo makuu matatu; ambayo ni mauzo, shoo za kimataifa na maendeleo yatokanayo na muziki.
Diamond, aliyetoka kimuziki mwaka 2009 ameshinda tuzo za kimataifa kama Channel O, MTV, Soundcity, Headies, Afrima, Afrimma, Kora, AEA, EAUSA, the HiPipo Music Awards n.k na kumfanya kuwa msanii pekee Bongo kufikia mafanikio hayo kwa kipindi cha miaka 10.
Anashikilia rekodi ya kushinda tuzo saba za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) 2014 kwa usiku mmoja, anakaribiwa na Alikiba aliyeshinda tuzo tano mwaka 2015, ikiwa ni sawa na asilimia 20 kwa mwaka 2011.
Ndiye msanii wa kwanza Bongo kuchaguliwa kuwania tuzo za BET katika kipengele cha Best International Act, tayari amewania mara tatu (2014, 2016 na 2021) na kumfanya kuwa msanii pekee Bongo aliyewania mara nyingi.
Diamond ameweza kushinda na kutunukiwa tuzo zaidi ya 46 za ndani na za kimataifa, huku akimpiku Lady Jaydee mwenye tuzo zaidi ya 35.
Ndani ya muda huo ametoa albamu tatu, Kamwambie (2010), Lala Salama (2012), A Boy From Tandale (2018), pamoja na Extended Playlist (EP), First of All (2022), akiwa msanii pekee aliyefanikiwa kufanya hivyo.
Diamond ndiye msanii pekee katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara aliyevutia watazamaji zaidi ya bilioni 1.7 YouTube na kujikusanyia wafuasi zaidi ya milioni 6.3.