Baadhi ya wajumbe wanaodaiwa kushiriki katika kumteua Steven Nyerere kuwa msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzani (SMT), wamekana bodi kuhusika kufanya uteuzi huo.
Wajumbe hao ni Whitney Kibonge Mwepesi na Msanii wa Hiphop, Bahgdadi, ambapo wanaelezwa kushiriki katika kikao cha uteuzi huo.
Wakizungunza kwa nyakati tofauti, Whitney amesema kikao walichoketi kilikuwa ni cha kawaida na si cha bodi ambacho hutolewa kwa barua rasmi zinazowekwa kwa ajili ya kumbukumbu.
“Naomba niliweke hili wazi kikao hakikuwa cha bodi, nilitwa kwa simu kwamba kuna kikao cha kawaida na moja ya ajenda ilikuwa kuzungumzia masuala ya tuzo na kingine kuzungumza na Katibu wa Wizara ambaye alifanya hivyo kwa njia ya simu,mazungumzo ambayo sio sahihi kuasema hadharani kwa kuwa ni mambo ya ndani ya Shirikisho.
” Hata kabla hatujaondoka ajenda ya mwisho ikapenyezwa ya kuletwa jina la Steve kuwa msemaji lakini tuliambiwa ni siri kwanza mpaka hapo maoni yatakapokusanywa kwa wanachama kama wanamkubali au la lakini wakati huo Steve tuliona Rais akipigia simu kumtaarifu kuwa ameteuliwa.
“Ajabu wiki iliyopita nilishangaa naona viongozi wenzangu, wameitisha mkutano na waandishi wa habari na kumtangaza Steve kuwa msemaji, sikuonekana katika kikao hicho na wala kile cha dharura cha kusikiliza maoni ya mwanachama juzi sikutokea,kwa kuwa naona kilichofanyika sicho tulichokubaliana”, amesema Whitney aliyewahi kutesa na kundi la Wakilisha.
Kwa upande wake Baghdad amesema kikao walichoketi wiki iliyopita haikukuwa cha bodi na yeye alikuwa akimwakilisha Katibu wake wa Tuma, Sogy Doggy na ilikuwa apeleke yaliyojadiliwa kwake.
Baghdad amesema ataendelea kusimamia haki kama wanachama wengi katika Shirikisho wakiona Steve anawafaa kuwa msemaji hatakuwa na pingamizi.