Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amesisitiza kuwa, yupo kwenye penzi zito na mpenzi wake mpya licha ya kumtaja mchumba wake huyo.

Diamond amedai kwamba, katika penzi alilopo kwa sasa analishwa vinono na mpenzi wake huyo mpya ambaye amemficha kumtaja.

Diamond ameendelea kukanusha madai ya kumchumbia msanii wake, Zuchu ambaye yupo chini ya lebo yake ya Wasafi.

“Niko kwenye mahusiano na nina furaha. Ninafurahia mahusiano yangu, yananipa raha na amani, huba limetaradadi,” anasema Diamond wakati huu akiendelea kuitangaza albam yake fupi (EP) ya First Of All (FOA).

Diamond anasema kuwa, anampenda mchumba wake kwa kiasi kuwa anakosa maneno ya kutumia kuelezea hisia zake.

“Nampenda sana naye anafahamu nampenda na maneno tupu hayatoshelezi ila matendo yangu yeye anayaona,” anaongeza Diamond.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *