Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA amelazimika kutoa tamko rasmi kwa niaba ya wasanii wenzake juu ya uteuzi wa Steve Nyerere kuwa Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT).

Mwana FA ambaye aliwahi kuwa Kiongozi wa Chama Cha Muziki wa Kizazi Kipya (TUMA) ameipa Bodi ya Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT) saa 48 wawe wamekaa na kutoa suluhu ya jambo.

Mwana FA amesema kuwa, uteuzi wa Steve Nyerere umekiuka taratibu za upatikanaje wake kwa kuwa hana vigezo vinavyohitaji ili mtu awe msemaji wa shirikisho hilo.

Wasanii wameonekana kutopendezwa na uteuzi wa Steve Nyerere kuwa msemaji wa Shirikisho la muziki nchini Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *