Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Jux amekuwa msanii wa kiume aliojitokeza kwenye vipengele vingi katika Tuzo za Muziki za Tanzania (TMA) 2021.
Wateule wa tuzo hizo wametangazwa siku ya Jumamosi Machi 20, 2022 na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), huku Nandy na Jux wakionekana kung’ara katika vipengele vingi kila mmoja kati ya 51 vinavyoshindaniwa
Kwa upande wa Nandy ametajwa kwenye vipengele saba, amejitokeza katika kipengele cha msanii bora wa kike wa Bongo Fleva akichuana na wakina Anjella kutoka lebo ya Konde Gang, Rosa Ree, Saraphina na Marry G.
Kipengele kingine alichochomoza msanii huyo ni wimbo bora wa wa msanii wa kike, mwanamuziki bora wa kike, mtumbuizaji bora wa kike, chaguo la watu, msanii bora Afrika mashariki na wimbo bora wa kushirikiana kupitia wimbo wake wa leo leo aliomshirikisha mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kongo, Koffi Olomide.
Kwa upande wa Jux ametajwa katika kipengele cha msanii bora wa kiume wa Bongofleva akichuana na akina Harmonize, Marioo, Whozu na Ben Pol.
Pia yupo katika kipengele cha mwanamuziki bora wa kiume wa mwaka, akishindanishwa na Profesa Jay, Young Lunya, Ben Pol na Harmonize.
Aidha yupo Katika kipengele cha wimbo wa kushirikiana kupitia wimbo wake wa Lala alioimba na msanii Rayvanny, video bora na chaguo la watu.
Tuzo za muziki zinatarajiwa kutolewa Aprili 1, 2022, huku vigezo vikubwa vilivyotumika kuwapata watu vikiwa ni wale waliopeleka kazi zao, waliosajiliwa Cosota na Basata na kubwa kamati kuwachagua kwa kuwaona wanafaa.