Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nandy amefunguka na kusema kuwa hajawahi kugombana na Wema Sepetu Sepetu na wala hajawahi kumchukulia bwana kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakiongea.
Nandy amesema kuwa kipindi cha nyuma kuna maneno mengi yalisambaa mitandaoni, kwamba yeye na Wema ni kama paka na panya kutokana na kile kilichodaiwa kwamba, eti wameibiana mabwana, jambo ambalo mwenyewe anasema halikuwa na ukweli wowote.
Nandy amesema kuwa “Huwezi kuamini, mimi na Wema hatujawahi kugombana kabisa, nilikuwa nashangaa wanavyosema eti nilimuibia bwana ake, kitu ambacho hakina ukweli wowote, siwezi kufanya hivyo,
Pia Nandy amesema kuwa Watu huwa wanaongea sana, halafu wanaongea mambo wasiyokuwa na uhakika nayo, nampenda Wema na sitaacha kufanya hivyo, zaidi tunasapotiana sana kwenye kazi,”.