Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Damian Soul ameshangazwa na kitendo cha waandaaji wa tuzo za Tanzania (TMA) kumuweka kwenye kipengele cha msanii bora chipukizi.

Damian akisema hayo baada ya Basata inatangaza matokeo hayo walikumbana na maswali ya waandishi kwa nini wamemuweka kipengele hiko, walisema alijichagulia wakati wa kuwasilisha kazi yake.

Damian amesema hajaridhika na kipengele alichopangwa na alichoamua ni kujiondoa kwenye mashindano hayo kwa kuwa kipengele alichowekwa sicho alichojipendekeza kama masharti waliyokuwa wamepewa ya msanii kujiweka anapoona anafaa.

Katika kipengele cha chipukizi, Damian anashindanishwa na wasanii Kusah, Lody Music, Rapcha na Knata MC anayeimba nyimbo za singeli.

Katika kulipinga hilo, Damian anabainisha kuwa “Kupitia kampuni ninayofanya nayo kazi zangu za muziki ya Slide Vision, nilijipendekeza kwenye kipengele cha wimbo bora wa mwaka nikiamini kibao changu cha mapopo ndipo kilistahili hapo.

“Huku ni kunikosea kikubwa na kunidhalilisha mbele ya mashabiki zangu ambao wanajua uwezo wangu, naomba niseme sitaki kushiriki hizo tuzo zao,” amesema Damian aliyetingisha na kibao hiko cha mapopo kilicho katika mahadhi ya amapiano na kutesa sana kwa mwaka 2021.

Tuzo za TMA zinatarajiwa kutolewa Aprili 1, mwaka huu ikiwa imepita miaka sita kusitishwa kutolewa kwa tuzo za muziki nchini, huku kipengele 51 vikiwa vinawaniwa na wasanii wanaofanya muziki wa aina mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *