Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny takriban siku kumi yupo jijini Paris nchini Ufaransa kwa shughuli za kimuziki.

Rayvanny au Vanny Boy amekuwa studio na wasanii mbalimbali kama Adenkule Gold wa Nigeria ikiwa ni muendelezo wa kolabo zake za kimataifa.

Rayvanny amesema kuwa anakaa kwenye hoteli ambayo analazimika kulipia shilingi milioni 2 za Kitanzania kwa siku hivyo kwa siku kumi alizokaa nchini humo zimemtoka shilingi milioni 20.

Rayvanny ameandika; “Imagine nipo hapa (hotelini) toka tarehe 7 (Machi), 2 milioni kwa siku chumba…”

Hata hivyo, hiyo inaweza isiwe habari kubwa kwani Diamond Platnumz; ambaye ni bosi wake kunako Lebo ya WCB anasema Rayvanny ndiye msanii wa pili kwenye lebo hiyo anayeingiza pesa nyingi Zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *