Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameonesha kutounga mkono uteuzi wa muigizaji Steve Nyerere kuwa msemaji wa shirikisho la muziki nchini.
Kupitia Insta Story, Diamond ameanza kwa kuandika “Serikali ina nia njema sana ya kukuza sanaa, ila inatakiwa kuwa makini sana na watu wanaowateua kusimamia nyanja mbalimbali katika Tasnia zetu, Maana watu hao wanachokifanya ni kulidharirisha Taifa na kufanya Taifa letu lionekane halina Weledi” -Diamond Platnumz
Fid Q mbele ya cameras unatabasamu ila najua kabisa ukikaa pekeyako unajuta na kujua kuwa umejivunjia Heshima kubwa uloijenga kwa Muda Mrefu!…wewe ni ICON usikubali kupoteza Legacy uloijenga kwa Maumivu na jasho kisa Mihemko, pasi na kutumia fikra”.
“Muziki ni Kazi, Muziki ni Ajira, Muziki ni Mkombozi wa vijana wengi ambao leo hii wanasaidia familia zao, lakini pia kuchangia Pato la Taifa.
Muziki Unatangaza Tamaduni na Kuleta Heshima na Sifa Nchini Kuichezea sanaa ni kuichezea Nchi kwenye ujira wa vijana wengi
Sanaa hii, ilindwe, iheshimike, isaidiwe kuwa na watu makini ili kuikuza zaidi na kuwezesha kazi zetu kuuza kimataifa na kulinda soko kubwa la ndani ambalo wenzetu wa nje kila siku wanalitamani kuja hapa kuchukua pato letu.
Pia amemalizia kwa kuandika kuwa Raisi wetu Mh. Samia Suluhu Hassan anapambana Usiku na mchana kutuletea Maendeleo ambayo tuliyalilia kwa Muda Mrefu kwenye sanaa… Tuyatumie vizuri Mambo hayo na sio Kumsononesha!”.