Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amefunguka na kusema kuwa mpenzi wake Briana namfundisha lugha ya kingereza timu mana siku hizi anajua kuongoea lugha hiyo.
Safari hii anaeleza namna ambavyo yeye si mtaalam wa lugha ya Kingereza isipokuwa mpenzi wake wa sasa, Briana anamsaidia kwenye eneo hilo kuliko ilivyokuwa kwa mpenzi wake aliyepita, Sarah.
Anasema; “Mimi siyo mtaalam sana kwenye Kingereza ila mtu akiongea namuelewa. Kingereza siyo lugha yetu, lakini cha msingi ni kujiamini tu!
“Mimi nimetokea mtaani, elimu yangu ni darasa la saba, sijaenda kozi yoyote ya kizungu! Mpenzi wangu Briana na yeye pia ananisaidia sana, siyo kama ilivyokuwa kwa Sarah kwa sababu Sarah na yeye Kingereza chake hakikuwa kizuri sana…”
Harmonize amekuwa akipendelea matumizi ya Kingereza kwenye nyimbo zake akiamini kuwa lugha hiyo inasaidia kuufikisha muziki wake mbali kimataifa.