Baada ya kusambaa kwa video yake chafu akicheza vibaya na msanii Gigy Money, hatimaye mpiapicha wa Diamond Platnumz, Lukamba ameamua kumuomba msamaha mkewe, Cecy.

Tukio hilo limejiri kwenye boti wakati Diamond akiendelea kuitangaza EP yake ya First Of All (FOA) ambapo yeye na timu yake walikuwa wakijiachia kwenye boti ndani ya Bahari ya Hindi.

Lukamba anasema alichofanya ni ujinga na siyo ujana hivyo anamuomba radhi mkewe kwa kuwa hayupo tayari kumpoteza.

Lukamba amemuandikia; “Mke wangu nakiri nimekukosea, mara nyingine unapokuwa kwenye mazingira fulani unajisahau na kwenda na vibe iliyopo. Nimejifunza, nakubali nilichokifanya ni upumbavu na siko proud nao na hakuna mwanamke yeyote angependezwa kuona mwanaume wake tena mume wa ndoa anafanya nilichokifanya, nisamehe mke wangu.

“Ule siyo ujana, ni ujinga nimefanya na naomba radhi kwako, nakupenda sana mke wangu na siko tayari kukupoteza, nimekukosea mbele za watu na ndiomana nakuomba msamaha wazi mbele za watu, nisamehe mama.”

Kwa kuweka rekodi vizuri, Cecy ni mke wa pili wa Lukamba baada ya kuachana na mkewe wa kwanza aitwaye Shuu Mimi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *