Mwanamitindo ambaye pia ni msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto anefunguka kuwa, kamwe hawezi kumshauri mtu yeyote juu ya uhusiano wake wa kimapenzi.

Hamisa anasema kuwa, katika mambo ya uhusiano wa kimapenzi ni vigumu kumshauri mtu hata siku moja kwa sababu hata yeye alipokuwa kwenye mapenzi walijitokeza watu mbalimbali na kumshauri, lakini hakuwaelewa, badala yake akaendelea na mambo yake.

“Kwenye mapenzi siwezi kumshauri mtu yeyote hata rafiki yangu wa damu maana ni jambo ambalo ni gumu kumwambia mtu akakuelewa’.

Pia amesema kuwa kwa sababu hata yeye walijaribu kunishauri nilipokuwa kwenye uhusiano wangu na ilishindikana mpaka mwenyewe nilipoamua kufanya uamuzi wangu,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *