Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuhu Mziwanda ametoa dukuduku lake moyoni kwa kuomba afunguliwe alipofungwa kwa sababu anateseka na familia inamtegemea.
Kwenye page yake ya Instagram Nuh Mziwanda ameandika kwamba “Sipendi bifu wala ugomvi ndio mana napenda sana amani na kuongea ukweli wa Moyo wangu bila kujali mtu mwingine atanichukulia vipi.
Pia ameandika ila ukiona unataka amani na bado mtu ana vita ya kukudidimiza ujue unaelekea kwenye unyonge na kuonewa huruma kama Ukraine”.
“Naomba kanifungue niwe free tena kama zamani, usinifungie nateseka sana nina familia yangu inanitegemea na sihitaji mapenz na wewe nahitaji ukanifungue tu”.