Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Anjella amefunguka mipango yake ya kufikia ndoto zake ambayo inafanana na njia walizopita wasanii wenzake, Nandy na Zuchu.

Anjella amesema kuwa, mbali na kufanya muziki mzuri kama wao, pia amepanga kuanzisha matamasha yake kama ilivyo kwa Nandy Festival au Zuchu Coming Home ambayo kama mipango itaenda sawa, yataanza mwaka huu.

“Shoo zangu mwaka huu zitakuwepo na wakati ukifika nitawaambia, ishu ni mipango tu, ikikaa sawa nitawaambia mashabiki wangu,” anasema Anjella.

Mwanamuziki huyo ameendelea kufanya vizuri toka ajiunge na lebo ya Konde Gang inayomilikiwa na mwanamuziki mwenzake, Harmonize.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *