Mwanamuziki wa Bongo Movies, Monalisa ameshusha pumzi kuashiria kushuka kwa presha baada ya kuhakikishiwa kwamba bintio yake yupo salama na amefanikiwa kutoka nje ya Ukraine kwenye vita kali kutokana na mashambulizi ya Urusi.

Monalisa ameandika; “Mungu wetu ametenda tena!! Sasa, naweza kula chakula kikashuka, naweza kujilaza nikapata usingizi maana binti yangu yupo salama nje ya mipaka ya nchi ya Ukraine.

“Alifanikiwa jana usiku kuingia nchi ya jirani yeye na wenzie wachache na wapo salama.
“Napenda kuwashukuru wote waliokuwa nasi katika kipindi kigumu ambacho tumepitia,hakika kilikuwa kipindi kigumu hasa, kama haukuwa na ndugu yoyote Ukraine ulikuwa unaona kama kichekesho tu kinachoendelea kwakuwa pengine sisi Tanzania (ikiwemo mimi mwenyewe) hatujawahi kujua hasa maana halisi ya neno vita na tuendelee kuombea sana Taifa letu katika hili.

“Kwa kipindi hiki, nimepata marafiki wapya hususan Watanzania waishio nje ya Tanzania nawashukuru sana.

“Lakini pia nimepata kusoma comments ambazo sijawahi kusoma wala kuwaza binadamu anaweza kumuwazia binadamu mwenzie tena waziwazi kweupe. Mojawapo ni hii, Putin mbona anachelewa kulipua bomu Sonia afe? Huu ni zaidi ya uchawi.

“Ila comments hizi zinanifanya nizidi kuamini kwamba binti yangu ana kitu cha ziada na cha kipekee na nikuambie wewe unaye-comment hivi usidhani unamuumiza bali unamjenga kuwa jasiri zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *