Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amejikuta pabaya mara baada ya kukosolewa vikali na wadau mbalimbali wanaosimamia haki za watoto nchini.
Ukolowaji huo umekuja kufuatia Harmonize kupanda stejin usiku na mtoto wake wa kike Zuuh katika tamasha lake la Afro East Carnival lilifanyika wekeend iliyopita.
Inasemekana msanii huyo kwa sasa anasakwa na mamlaka za Ustawi wa Jamii wilaya ya kinondoni, kufuatia kitendo chake hicho cha kuambatana na kumpandisha mtoto mdogo katika tamasha lililo fanyika usiku mkubwa.
Mwanamuziki huyo alikuwa na familia yake kwenye tamasha hilo lilohudhuriwa na mashabiki kibao nchini pamoja na watu wake wa karibu wakiwemo baba na mama yake mzazi.
Tamasha hilo lilifanyika katika uwanja wa Tabata Shule jijini Dar es Salaam ambapo Harmonize alikuwa na baadhi ya wasanii waliotumbuiza kwenye tamasha hilo.