Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema baada ya mapito ya muda mrefu amebadili mfumo wake wa maisha na kwamba anafanya dua na kumtegemea Mungu katika mambo yote.

Wema amesema pamoja na kubadili mfumo wa maisha yake bado ni yuleyule hajawahi kubadilika na anaamini katika kupata kwa wakati sahihi wa Mungu na sasa anaona huo wakati wake umefika.

“Mimi ni binti wa Kiislam nafanya sana dua. Watu wanamuona Wema wa mtandaoni, lakini binadamu tunakuwa na tunajifunza, tunaoamini katika Mungu.

Pia ameendelea kusema kuwa Mungu hukupa kwa wakati wake na wakati ambapo hakunipa aliwapa wengine, riziki inaenda kwa mzunguko,”.

Wema ni muigizaji wa siku nyingi katika tasnia ya Bongo Movie na ameigizaji filamu mbalimbali na waigizaji wa ndani nan je ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *