Muigizaji wa Bongo Movie, Irene Uwoya amefunguka na kusema kuwa anachukia sana watu kumuita jini mitandaoni wakati yeye ni binadamu wa kawaida.
Uwoya amesema kuwa, hii ni kwa sababu jina hilo linaweza kukua na kumtengenezea vitu tofauti kabisa katika maisha yake kwa sababu siku zote maneno yanaumba.
Muigizaji huyo maarufu nchini amesema kuwa kuitwa jina hilo kuna uwezekano mkubwa hata hao majini wenyewe wanaweza kumfuata na kumsababishia matatizo mengine makubwa maishani mwake.
“Yaani kiukweli kabisa hakuna jina ambalo ninalichukia kama kuitwa Jini. Kwanza linaweza kuathiri kabisa maisha yangu ya kila siku,” Alisema Uwoya
Muigizaji huyo kwasasa anatesa kwa kula maisha baada ya kuonekana sehemu kibao akitumia pesa na rafiki zake mbalimbali.