Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amekumbana na ukosolewaji mkali mtandaoni mara baada ya video ya wimbo wake mpya ‘Gidi’ kuonyesha bendera ya kibaguzi, ‘Confederate flag’ ya nchini Marekani.

Katika video hiyo iliyotoka Februari 18, 2022, bendera hiyo inaonekana kwenye sekunde ya 32 kwa udogo sana, ingawa kwenye picha zilizopigwa wakati video hiyo ikitengenezwa ndipo imeonekana sana.

Wakosoaji wameeleza kuwa hilo linaweza kuibua hisia kali dhidi ya Wamarekani hasa weusi ambao wamekuwa wakifuatilia muziki wake na hilo linaweza kuharibu biashara yake nchini humo.

Ijue Confederate flag

Ukweli ni kwamba bendera hiyo ikionekana popote pale inatoa ujumbe unaosema kuwa wazungu ni watu wenye thamani kuliko watu wengine wenye rangi ya ngozi tofauti  nao. Wenyewe wanaita ‘White Supremacy’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *